Kuhusu Maadili haya

Tunafanya shughuli zetu kwa viwango vya juu vya tabia za kimaadili na tunatarajia wafanyakazi wote, washirika wetu wote wa biashara, na kila mtu anayefanya kazi kwa niaba yetu duniani kote kuwa na mwenendo unaolingana na viwango hivi. Kuzingatia hili ni muhimu sana katika kuendeleza sifa yetu nzuri ya kuwa kampuni inayowajibika na kupata mafanikio endelevu ya biashara.

Mwongozo wa Maadili yetu ya Kazi unatumika kwa watu wote ulimwenguni katika uhusiano wa ajira na mashirika/kampuni zote za JTI, pamoja na wafanyakazi wa nje, kama wafanyakazi wa muda mfupi, hata kama hawajaajiriwa moja kwa moja na JTI.

Viwango vilivyotajwa katika Mwongozo wa Maadili yetu si kamilifu. Havichukui nafasi ya sheria za nchi au miongozo ya uendeshaji, sera na kanuni za kazi za JTI. Kama mwongozo ndani ya Maadili haya unatofautiana na sheria zinazohusika, mwongozo mkali zaidi utatumika ilimradi kufanya hivyo hakuvunji sheria husika.

Kushindwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Kazi ya JTI, wajibu wetu wa kisheria au miongozo yetu ya uendeshaji, sera na kanuni za kazi kunaweza kusababisha hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya mfanyakazi.

Tunataka kufanya biashara na washirika wanaokubali maadili yetu, kuzingatia na kufuata kwa uwazi viwango vilivyoainishwa katika Maadili yetu ya kazi.

Kila kipengele cha Mwongozo huu, kina kiunganisho cha taarifa za ziada kimetolewa, pamoja na:

Nani wa kuongea naye ukiwa na swali au nung'uniko.
Marejeo na kiunganisho cha sera na kanuni husika.
Kiunganisho cha rasilimali nyingine, zinazopatikana kwenye mtandao wa ndani wa JTI au kwenye mtandao.
Kiunganisho cha sehemu nyingine zinazohusika ndani ya Maadili haya.

Ingawa tafsiri za Mwongozo huu wa Maadili inaweza kufanyika, toleo la mwanzo la Kiingereza linabaki kua toleo rasmi.

Toleo hili la Mwongozo wa Maadili, litakalotumika mwezi Juni 2018, linachukua nafasi ya matoleo yote ya awali yaliyochapishwa na ya kielektroni. Mwongozo huu wa Maadili utapitiwa na kuboreshwa mara kwa mara.

Kilichopita Utambulisho kutoka kwa Afisa Maadili Mkuu
Kinachofuata Wajibu wako kama meneja