Uadilifu wetu wa biashara

Kutoa au kupokea zawadi, ukarimu na burudani

Hatuhimizi kutoa au kupokea zawadi, ukarimu na burudani ('GHE'), lakini tunatambua kwamba katika kufanya shughuli za biashara GHE hutokea.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Zawadi ni kitu chochote cha thamani unachopewa au kupokea bila kulipia. Ukarimu ni burudani pamoja na matukio ambayo yameshalipiwa, malazi, chakula na vinywaji.

Tunapaswa kuwa wazi wakati wa kupeana zawadi, ukarimu na burudani, kwa kuwa hizi zinaweza kuonekana kama rushwa au mgongano wa maslahi.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nafuata kanuni za GHE kabla ya kutoa au kupokea zawadi, ukarimu au burudani ya aina yoyote.

Siruhusu zawadi, ukarimu au burudani kuathiri maamuzi yangu ya biashara.

Kutoa au kupokea zawadi, ukarimu au burudani ya aina yoyote na afisa wa serikali au shirika la kiserikali, bila kujali thamani, lazima iidhinishwe.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Washirika wa biashara waliochaguliwa kufanya kazi kwa niaba yetu wanatakiwa kuzingatia kanuni zetu za GHE na kuomba idhini mapema pale ambapo watatoa au kupokea zawadi, ukarimu an burudani.

Kulingana na kanuni zetu za GHE, kupokea au kutoa zawadi, ukarimu na burudani lazima:

  1. Kuendanae na sheria na desturi za nchi husika.
  2. Kuwe kwa busara na uwiano, kuwe mara kadhaa tu na iwe pale ambapo inafaa tu.
  3. Kusilete mgongano wa maslahi kati ya wafanyakazi na watoa huduma wetu.
  4. Kusitolewe ili kupata faida isiyofaa, au kulipa au kushawishi, utendaji usiofaa.
  5. Kusiwe kwa pesa taslimu, vocha za manunuzi, au kuponi ambazo zinaweza kubadilishwa kuwa fedha.
  6. Kufafanuliwe ili kupata idhini. Ufafanuzi lazima uonyeshe dhumuni, gharama kamili ya GHE, na uorodheshe washiriki wote, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa JTI.

Fahamu zaidi