Uadilifu wetu wa biashara

Kusimamia mawasiliano ya nje

Wakati wafanyakazi waliopewa mamlaka ya kuongea na waandishi wa habari kwa niaba ya JTI, tu ndio walioruhusiwa kufanya hivyo, wafanyakazi wote wanahimizwa kushiriki katika vyombo vya habari vya kijamii vinavyohusiana na biashara yetu.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Uongozi wa juu wa JTI, wakurugenzi wakuu wa nchi mbalimbali na waliopewa mamlaka, wawakilishi wa kanda na wa nchini wa Maendeleo na Mahusiano ya Kampuni pekee ndio wanaweza kuzungumza na waandishi wa habari.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nakuwa makini sana kwenye kutoa taarifa JTI kwenye vyombo vya habari vya kijamii, taarifa pekee ninazotoa ni zile zilizotolewa na Kampuni na ambazo zinapatikana kwa ajili ya watu wote.

Siweki taarifa za siri kuhusu JTI kwenye vyombo vya habari vya kijamii, blogu, au kwenye majukwaa ya kuchati.

Kanuni kuu ni kwamba, kama sitaki kuona kitu kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la kitaifa, sipaswi kukiandika au kukitoa kwenye vyombo vya habari vya kijamii au katika jukwaa lolote la kijamii.

Vitu vya kufanya na kutofanya kwenye vyombo vya habari vya kijamii

  • NDIO – kuweka kwenye mtandao wako binafsi machapisho au kazi ambazo zimechapishwa kwenye vyombo vya mawasiliano vya biashara vya JTI.
  • NDIO – kuweka bayana kwamba hayo maoni ni yako kwako mwenyewe.
  • HAPANA – kuchapisha taarifa za siri kwenye vyombo vya habari vya kijamii.
  • HAPANA – kutangaza bidhaa za tumbaku za JTI kwenye vyombo vya habari vya kijamii.

Fahamu zaidi