Uadilifu wetu wa biashara

Kuzuia uhalifu wa kifedha

Tunapambana kuzuia hatari zinazohusiana na uhalifu wa kifedha.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Uhalifu wa kifedha unaidhuru jamii na serikali na inaweza kuathiri vibaya biashara na sifa ya JTI.

Uhalifu wa kifedha ni pamoja na utakatishaji wa fedha, ukwepaji kodi na kusaidia ukwepaji kodi. Utakatishaji fedha ni mchakato wa kuingiza fedha zilizopatikana kinyume cha sheria kwenye mzunguko wa fedha halali au mali nyingine. Kusaidia ukwepaji kodi ni kumsaidia mshirika wa biashara au mtoa huduma kukwepa kulipa kodi.

Adhabu za kukwepa kulipa kodi au kusaidia wengine kukwepa kulipa kodi zinaweza kuwa kali sana kwa JTI na wafanyakazi wake, hata kama JTI au mtu anayehusika hawakufaidika kutokana na shughuli zilizofanywa. Unaweza kuwajibishwa endapo utamsaidia kufanya shughuli hizo kwa kukusudia au bila kukusudia.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Sipaswi kushiriki au kusaidia aina yoyote ya uhalifu wa kifedha.

Sera ya Kupambana na Utakatishaji Fedha ya JTI ('AML') inafafanua sheria ya malipo ya ndani na ya nje ya biashara na inaweza kunisaidia kuhakikisha kuwa sisaidii utakatishaji fedha.

Nikiombwa kufanya kitu ambacho kinaweza kupelekea ukwepaji kodi au utakatishaji wa fedha, nakataa na kutoa taarifa mara moja.

Nikihisi mfanyakazi mwenzangu au mshirika wa biashara anashiriki kwenye uhalifu wa kifedha, natoa taarifa.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Tunatarajia washirika wetu wa biashara, ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya kazi kwa niaba yetu, kuzingatia kikamilifu kwamba JTI haivumilii uhalifu wa kifedha hata kidogo.

Tutafanya haki yetu ya kukomesha mipango ya mikataba ambapo washirika wa biashara wanahusika katika aina yoyote ya uhalifu wa kifedha.

Mshirika wa biashara akiombwa kufanya kitu ambacho kinaweza kusababisha uhalifu wa kifedha, anapaswa kutoa taarifa mara moja kupitia onebehavior@jti.com.

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Hii ni baadhi ya mifano ya uhalifu wa kifedha unaoweza kutokea:

  • Mshirika wa biashara ameniomba alipwe kupitia akaunti ya benki ya nje ya nchi iliyosajiliwa kwa mtoa huduma nisiyemjua na ninahisi sababu ya ombi hili ni kukwepa kodi.
  • Mteja ameniomba nibadilishe aina ya bidhaa walizonunua kwenye ankara zao ili kupunguza kiwango cha kodi ya ongezeko la thamani - VAT au kodi au malipo mengine.

Fahamu zaidi