Uadilifu wetu wa biashara

Kutoa na kutunza taarifa za Kampuni

Biashara yetu inategemea ukweli, haki, wakati na usahihi wa kuhifadhi kumbukumbu ili kusaidia kwenye kufanya maamuzi yetu, kulinda sifa yetu, kukuza ufanisi wa uendeshaji na kukidhi majukumu ya kisheria na udhibiti.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Taarifa za Kampuni ni pamoja na taarifa za kifedha na za uendeshaji, taarifa binafsi na za siri, kumbukumbu za mikutano, mipango ya biashara, utabiri na uchambuzi.

Kumbukumbu za biashara na za fedha ni muhimu kwa shughuli zetu za biashara na ushiriki wetu na wanahisa wetu, washirika wa biashara, serikali na wadau wengine.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nahakikisha kwamba kumbukumbu zimehifadhiwa kwa siri, salama na zinaweza kupatikana na zinaheshimu sheria zinazofaa na kanuni kwenye utunzaji na utumiaji wake.

Nikihusishwa kwenye kutoa taarifa za kampuni za fedha au kuweka kumbukumbu, nafuata kanuni za uhasibu zilizokubalika na kuhakikisha kuwa kumbukumbu ni sahihi, salama na zimehifadhiwa salama zitakapohitajika kutumika.

Kama nimefanya makosa kwenye kutoa au nimeshindwa kutoa kitu ambacho kinaweza kuathiri uadilifu na uaminifu wa kumbukumbu za kampuni, natoa taarifa mara moja kwa Afisa Mkuu wa Fedha, Mdhibiti wa Kampuni au meneja wangu.

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Hii ni baadhi ya mifano ya mazingira ya kutilia shaka kuhusu taarifa za kifedha:

  • Taarifa za mapato ambayo bado hayajapatikana au gharama ambazo bado hazijafanyika.
  • Kushindwa kupata faida kutokana na gharama zilizopatikana katika mwaka wa taarifa.

Fahamu zaidi