Uadilifu wetu wa biashara

Kulinda mali za Kampuni

Mali za Kampuni za JTI ni muhimu kwa kutusaidia kufikia malengo yetu ya biashara. Tunatumia mali ya Kampuni ya JTI, na mali za wengine, kwa uangalifu na kwa heshima. Tunahakikisha kuwa mali zetu za Kampuni zinapatikana kwa usahihi, zinatunzwa, zinalindwa na kuhifadhiwa.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Mali ya Kampuni ni pamoja na mashine na vifaa, vifaa vya IT, bidhaa na vifaa vya uzalishaji, mali za kitaaluma (IP) na taarifa za Kampuni.

Matumizi mabaya, kutokuwepo au kuharibika kwa mali za Kampuni kunaweza kuharibu biashara yetu na kunaweza kusababisha hasara za kifedha na wa jina letu.

IP yetu ni muhimu sana kama inatusaidia kutofautisha bidhaa zetu na huduma na kudumisha faida ya ushindani. Uvumbuzi wote, mawazo na dhana zilizotengenezwa kwa ajili ya JTI na wafanyakazi wetu wakati wa ajira zao ni mali ya Kampuni na havipaswi kufanyiwa biashara kwa siri.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nina wajibu wa kulinda mali za Kampuni nilizopewa dhidi ya wizi, matumizi mabaya na uharibifu.

Natumia mali ya Kampuni kulingana na sera na taratibu za JTI na sizitumii kwa manufaa yangu binafsi. Situmii mali ya Kampuni, ikiwa ni pamoja na mali miliki, na wadau wa biashara bila idhini. Sichukui au kutumia mali za wadau wa biashara bila idhini maalum.

Kila ninapotaka kumpa mtoa huduma kazi kufanyia kazi taarifa za Kampuni, nahusisha timu ya IT. Hii itawawezesha kuhakikisha taarifa zetu iko salama.

Naelewa thamani na hatari iliyopo ya taarifa za kidigitali zisipolindwa na ninafuata kanuni za i-secure ili kupunguza hatari ya wizi au upotevu wa taarifa.

Nikiwa na shaka kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali za IT, nawaomba Global Service ('GSD') msaada. Nikifanya kosa, natoa taarifa mara moja.

Kumbuka kanuni muhimu za kanuni i-secure:

  • Nalinda taarifa iliyopo mtandaoni
  • Nafikiri kabla ya kubonyeza
  • Natoa taarifa kwa usalama/umakini
  • Ukiwa na maswali yoyote, muulize mtaalamu, kwa kuwasiliana na Timu yako ya IT, GSD au kwa kuwaandikia information.security@JTI.com.

Fahamu zaidi