Uadilifu wetu wa biashara

Kupambana na hongo na rushwa

Hatuvumilii hongo au rushwa ya aina yeyote.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Tumejitolea kufanya kazi kwa uaminifu katika shughuli zetu zote za biashara na kutovumilia hongo na rushwa katika nchi zote tunazofanyia shughuli zetu.

Hongo inahusisha kutoa au kupokea kitu cha thamani (kwa kawaida ni pesa) ili ufaidike kibiashara. Rushwa ni matumizi mabaya ya mamlaka kwa faida binafsi.

Malipo ya uwezeshaji ni aina ya hongo na kwa kawaida huhusisha zawadi ndogo au malipo kwa maafisa wa ofisi za umma ili wafanye au kuongeza kasi kwenye huduma ya kawaida.

Kuvunja sheria za hongo na rushwa kunaweza kusababisha uchunguzi wa uhalifu na mashitaka, pamoja na adhabu za kifedha kwa JTI na wafanyakazi wanaohusika.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi wa JTI?

Sishiriki katika aina yoyote ya hongo au rushwa. Hasa,nikiombwa kupokea au kutoa rushwa au malipo ya kuongeza kasi ya kazi kwenye huduma ya kawaida. Nakataa na kutoa taarifa mara moja kwa Mshauri wa Sheria wa kanda au wa nchini na kwa mjumbe wa timu ya kitengo cha Maadili.

Pia nakumbuka hatari za kutoa au kupokea zawadi, ukarimu, burudani na misaada kwa wahitaji na udhamini.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Tunatarajia washirika wetu wa biashara, ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya kazi kwa niaba yetu, kuzingatia kikamilifu kwamba JTI haivumilii hongo na rushwa kwenye kufanya biashara na JTI.

JTI inaweza kusitisha mkataba na mshirika yeyote wa biashara atakayehusika na aina yoyote ya rushwa au ufisadi.

Kuyaishi maadili yetu

"Nilipokea simu nyingi na barua pepe kutoka kwa wakala wa mauzo ambaye tunatarajia kufanya naye kazi. Nilimwambia bidhaa alizopendekeza hazikidhi viwango vyetu. Akanipigia simu tena, akisema kuwa yuko tayari kunilipa asilimia 5 ya ziada kama 'faida yangu binafsi’ ikiwa JTI itakubali ofa yake. Nilimwambia kwamba mambo hayo hayaendani na Maadili yetu ya Kazi, na kumwomba asipige simu JTI tena. Na nilimtaarifu meneja wangu mara moja."

Mfanyakazi wa PPO

Fahamu zaidi