Uadilifu wetu wa biashara

Kuheshimu vikwazo vya kiuchumi na udhibiti wa kuuza nje ya nchi

Tunahikikisha kwamba tunazingatia vikwazo vya kiuchumi vinavyofaa na udhibiti wa kuuza nje

Hii ina maana gani kwa JTI?

Vikwazo vya kiuchumi na udhibiti wa kuuza nje vinaweza kubana au kuzuia shughuli za biashara na watu maalumu, mashirika au nchi. Vinaweza pia kubana au kuzuia kuuza nje au kuagiza bidhaa au huduma fulani. Adhabu za ukiukwaji wa vikwazo vya udhibiti wa kuuza nje, hata bila ya kukusudia, inaweza kuwa kali kwa wote, JTI na wafanyakazi wake.

Tuna sera na taratibu za kusaidia kuhakikisha kuwa hakuna biashara au wafanyakazi anafanya shughuli na nchi zilizozuiliwa.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nina wajibu wa kujua na kuzingatia Sera za JTI za Vikwazo vya Kiuchumi na kuheshimu vikwazo vyote na udhibiti wa kuuza nje vinavyonihusu mimi au sehemu yoyote ya JTI ninapofanyia kazi.

Kwa shughuli za biashara zinazojumuisha nchi zilizowekewa vikwazo, bidhaa au huduma, naomba kwanza kibali cha maandishi kutoka kwa Mshauri Mkuu wa kitengo cha Maadili wa kanda yangu, Mshauri wa Sheria nchini au Afisa wa kitengo cha Vikwazo vya kiuchumi.

Nikiwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kupata kikwazo cha biashara au udhibiti wa kuuza nje, namjulisha Mwanasheria Mkuu wa kanda yangu, Mshauri wa Sheria nchini au Afisa wa kitengo cha Vikwazo vya kiuchumi mara moja.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Tunatarajia washirika wetu wa biashara watazingatia vikwazo vyote vinavyotumika na udhibiti wa kuuza nje na kwa Viwango vya Wasambazaji vya JTI.

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Haya ni baadhi ya mazingira ambapo vikwazo vya kiuchumi vinaweza kuwa hatarini kukiukwa:

  • Kama raia wa Marekani au mmiliki wa kadi ya kijani, nimeorodheshwa kama kibali cha BAP / Memo kwa ajili ya mradi unaohusiana na nchi iliyo chini ya Marekani.
  • Napenda kulipa wasambazaji kutoa bidhaa kwa nchi chini ya kibali cha Marekani kwa kutumia dola za kimarekani.
  • • Natamani kutuma kifaa cha mionzi kinachoweza kutumika kwa matumizi ya kiraia au ya kijeshi kwa kiwanda cha JTI, lakini sijathibitisha kama kibali kinahitajika.

Fahamu zaidi