Bidhaa zetu

Kuhakikisha ubora wa bidhaa

Tunajivunia kua shughuli zetu za uzalishaji ni za viwango vya Kimataifa, vinavyokidhi viwango vya ubora vya JTI na matarajio ya wavutaji.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Tunazalisha bidhaa kulingana na maelekezo maalumu ya kitaalamu, kwa kutumia tumbaku na malighafi nyingine kutoka kwa wazalishaji wanaoaminika.

Ubora unahakikishwa katika hatua zote za upatikanaji tumbaku na malighafi nyingine, uzalishaji, uhifadhi, usambazaji na huduma kwa wateja, kwa kufuata kwa ukamilifu matakwa yote ya kanuni za udhibiti wa tumbaku na kisheria.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Siku zote nafuata viwango na kanuni za ubora za JTI, bila kujali muda au vikwazo vingine vya rasilimali.

Nahakikisha washirika wowote wa biashara ninaofanya nao kazi wanafanya hivyo pia.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Tunatarajia washirika wetu wa biashara kuzingatia sheria zinazohusika, Viwango vya usambazaji vya JTI, vigezo vya ubora wa vifaa na mikataba ya huduma. Wanahitajika kupatikana kirahisi kwa ajili ya ukaguzi wa bidhaa na huduma wakiombwa na JTI.

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Hii ni baadhi ya mifano ya masuala yanayohusiana na ubora wa bidhaa:

  • Msambazaji amenitaarifu kwamba stempu ya kodi ya mapato haipo kwenye moja ya bidhaa zetu za kusafirishwa.
  • Baadhi ya paketi za sigara zipo tofauti na zilizochapishwa kwenye katoni.
  • Mteja ametoa taarifa kwamba pakiti za sigara zimefika bila tepu hivyo ana wasiwasi zinaweza kuwa zilifunguliwa au kuharibiwa.

Fahamu zaidi