Hii ina maana gani kwa JTI?
Tunalipa jukumu hili uzito na tunatii kikamilifu kanuni zote zinazofaa na Kanuni za Masoko za JT ulimwenguni kote.
Hatuuzi bidhaa zetu kwa watoto. Pia hatuhimizi mtu yeyote kuanza kuvuta sigara, na hatujaribu kuzuia wavutaji kuacha kuvuta. Tunauza bidhaa zetu kwa wavutaji watu wazima ili kudumisha uaminifu wa bidhaa yetu na kuhimiza wavutaji watu wazima wanaovuta bidhaa za mshindani kuhamia kwenye bidhaa zetu.
Tunaamini kwamba wavuta watu wazima wanapaswa kufahamu vizuri kuhusu hatari za uvutaji wa sigara kwa afya kabla ya kufanya uamuzi wa kuvuta sigara.