Bidhaa zetu

Kupambana na biashara haramu

Tunaongoza kwenye sekta katika kupambana na biashara haramu ya tumbaku kupitia ushirikiano wetu na vyombo vya kutekeleza sheria na serikali, pamoja na maendeleo ya teknolojia ya hali ya juu.

Hii ina maana gani kwa JTI?

JT Group inapinga kufanya biashara ya tumbaku kinyume cha sheria na inapambana na aina zote za biashara haramu hivyo inasambaza yenyewe na kufanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kutekeleza sheria ili kupambana na changamoto hii.

Tumbaku haramu hudhoofisha biashara halali ya tumbaku, inapunguza mapato ya serikali, na inachochea uhalifu.

Tunafuatilia masoko na wateja wetu kwa ukaribu ili kuhakikisha kuwa bidhaa za tumbaku za JTI zinawafikia watumiaji watu wazima kupitia njia za halali za biashara katika masoko yao yaliyokusudiwa.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Ili kusaidia jitihada za JTI za ugavi halali wa tumbaku, nahakikisha kwamba mshirika yeyote wa biashara ninayehusiana naye kikazi anatambua viwango vya uuzaji vya JTI na sera husika za JTI. Mshirika yeyote wa biashara anayenunua bidhaa zetu za tumbaku lazima awe na sifa na kupitia programu yetu ya kuchunguza wasambazaji ili kupata idhini ya kufanya kazi na sisi.

Nitatoa taarifa mara moja kwa Mjumbe wa timu za Kupambana na Biashara Haramu na wa timu ya kitengo cha Maadili nikiwa na shaka na mwenendo wa shughuli inayohusisha mshirika wa biashara wa JTI au bidhaa.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Tunatarajia washirika wetu wote wa biashara watailinda JTI na shughuli zake zote za biashara na uzalishaji dhidi ya aina yoyote ya biashara haramu. Aidha, tunatarajia ushirikiano kamili kutoka kwa washirika wetu wa biashara na wasambazaji wetu kuhusu programu yetu ya kutoa vyeti vya kuwaidhinisha kufanya kazi na Kampuni.

Timu yetu ya Kupambana na Biashara haramu inafanya kazi na mamlaka za utekelezaji sheria kuchunguza kukamatwa kwa bidhaa yoyote ya JTI. Uchunguzi ukibainisha sifa mbaya ya mshirika wetu yeyote wa biashara, tunachukua hatua inayofaa ili kuhakikisha kuokoa ugavi wetu, ikiwa ni pamoja na kusitisha mahusiano ya biashara ikibidi.

Kwa idadi

  • Sigara 1 kati ya 10 ulimwenguni ni haramu
  • Zaidi ya dola bilioni 40 za mapato ya kodi ya kimataifa zinapotea kila mwaka
  • Zaidi ya sigara haramu bilioni 1 (au sawa yake) zilikamatwa mwaka 2017, tunaushukuru ushirikiano wetu na mamlaka za utekelezaji sheria

Fahamu zaidi