Watu wetu

Kuhakikisha afya na usalama

Wafanyakazi wote wana haki ya kulindwa dhidi ya ajali kazini na magonjwa. Tunatoa mazingira ya kazi yaliyo salama na, tunaimarisha utamaduni unaoupa kipaumbele usalama wa watu na afya zao.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Tunafanya kazi pamoja ili kudumisha utamaduni wetu wa usalama na kuweka mazingira ya kufanyia kazi salama. Tunakuza ufahamu wa usalama na kujiongezea ujuzi na kuwa na zana za kutambua hatari, kuzuia matukio na kulinda afya ya wafanyakazi wote.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nahakikisha kwamba nahudhuria mafunzo yote ya Afya na Usalama na nazielewa taratibu na kanuni za afya na usalama za nchini/Kampuni.

Nawajibika kwa usalama wangu mwenyewe na wa wafanyakazi wenzangu. Nikitakiwa kutumia au kuendesha mashine au gari la Kampuni, ni lazima niwe makini na nihakikishe usalama na kukukumbuka hatari zinazoweza kutokea. Sipaswi kuendesha mashine, gari au kufanya shughuli nyingine yoyote ambayo inaweza kusababisha madhara kwangu au kwa wengine endapo uamuzi wangu au matendo yangu ni dhaifu au hayako sawasawa.

Natoa taarifa kukiwa na hali, tabia na matendo yasiyozingatia usalama na kosakosa za ajali.

Kama meneja, nina wajibu wa kujitoa kuongoza utamaduni wetu wa usalama. Nahakikisha kwamba wafanyakazi wana uwezo unaotakiwa, ujuzi, mafunzo na vifaa vya kufanya kazi kwa usalama. Nikiletewa tukio la afya na usalama au hatari inayoweza kutokea, nashughulikia mara moja

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Tunatarajia kwamba washirika wetu wa biashara watahakikisha wana mazingira ya kazi na hali inayodumisha usalama. Wanatakiwa kuwa na sera na mifumo ya kutosha ya kusimamia afya na usalama.

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Hii ni baadhi ya mifano ya hali za hatari zinazoweza kutokea:

  • Nina wasiwasi kwamba mfanyakazi mwenzangu anataka kuendesha au kutumia mashine akiwa amekunywa pombe.
  • Meneja wangu ameniomba kufanya kazi fulani, lakini sijawahi kupata mafunzo ya kutosha ya kufanya kazi hiyo kwa usalama.
  • Nimeona waya wa umeme ulioharibika ambao unaweza kuniumiza mimi au mwenzangu.

Fahamu zaidi