Watu wetu

Kuwapa watu usawa na heshima

Tunazingatia uanuwai na kukuza utamaduni wa kujumuisha watu wa aina mbalimbali ambapo kila mtu anaweza kubakia na uhalisia wa asili wake bila hatari ya kubaguliwa au kunyanyaswa.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Tabia zisizo na heshima, ubaguzi na unyanyasaji zinakinzana na maadili ya JTI, na tuna wajibu kwetu binafsi na kwa wengine wote wa kufanya kitu pale ambapo tunaona mambo hayako sawa.

Hatubagui au kuvumilia ubaguzi wa jinsia umri, asili, dini, ulemavu, mwelekeo wa kingono, hali ya ndoa ama la, kabila, utaifa au sifa bainifu nyingine yoyote inayoruhusiwa kisheria.

Hatuvumilii aina yoyote ya unyanyasaji au vitisho iwe kwa matendo, maneno au maandishi.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nathamini na kuheshimu tamaduni, maoni na mwenendo wa maisha unaotofautiana na wakwangu. Natambua namna ambavyo tabia yangu inaweza kuathiri wengine. Naepuka mawasiliano ya kukera, yenye fujo au ya kutisha wengine. Sifanyi vitendo au kutoa ishara za kimwili zinazoashiria ngono zisizowapendeza wengine.

Kama ni mvutaji wa sigara, naheshimu haki ya wasiovuta sigara ya kufanya kazi kwenye mazingira yasiyo ya moshi.

Endapo mtu yeyote ataonyesha tabia isiyokua ya heshima au aina yoyote ya ubaguzi au unyanyasaji kwangu, nahimizwa kutoa taarifa kwa meneja wangu, HR Business partner au kwa mjumbe wa timu ya kitengo cha Maadili.

Kama meneja, nakubali uanuwai na kuwatendea wengine kwa usawa na heshima. Nafanya maamuzi ambayo ni ya haki na yasiyo ya upendeleo. Sivumilii aina yoyote ya ubaguzi au unyanyasaji na nachukua hatua mara moja ninapoletewa taarifa pale ambapo mfanyakazi anakua na mashaka au wasiwasi.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Washirika wetu wa biashara wanatarajiwa kuzingatia hali ya kazi inayoruhusu wafanyakazi kufanya kazi kwenye mazingira ya kuheshimiwa na yenye kuzingatia usawa na kuhakikisha kuwa hakuna mfanyakazi anayepata aina yoyote ya ubaguzi au vitisho.

Hizi ni baadhi ya tabia zisizojali hisia za watu wengine:

  • Utani usiofaa, maoni ya hali ya ngono au maoni yasiyo na heshima kwa wanaume au wanawake
  • Kutoa maoni yanayodhirisha ubaguzi wa rangi
  • Kumdhalilisha mfanyakazi au kundi la wafanyakazi, kwa mfano kwa kuonyesha makosa yao mbele ya wengine
  • Kukandamiza watu au makundi ya watu, kwa mfano kwa kuwabagua kwenye shughuli au mazungumzo

Fahamu zaidi