Kutoa taarifa ukiwa na manung'uniko

Tuna jukumu la pamoja kudumisha haki, heshima na uadilifu katika shughuli tunazofanya baina yetu na wabia wetu wa biashara. Katika JTI, tunazipa uzito taarifa zote za manung'uniko na kuchukua hatua muhimu za kutatua.

Je, nimpe nani taarifa nikiwa na manung’uniko?

Ukiwa na manung’uniko, siku zote omba mwongozo. Kote kwenye Mwongozo huu, vipengele vya ‘Fahamu zaidi’ vinakuongoza kwenye idara husika ambayo itakusaidia ukiwa na maswali au kukupa maelezo zaidi.

Ukisikia au kuona jambo ambalo unaamini kwamba linakiuka sheria, linaweza kukiuka Maadili yetu ya kazi, sera au kanuni, au linaweza kutishia sifa yetu ya biashara, unapaswa kulizungumza.

Unaweza kuzungumza na meneja wako wa kazi au HR business partner nchini kwako kwa kujiamini kuhusu jambo lolote linalokukabili. Usipohisi amani kuongea na watu hawa, unaweza kutoa manung’uniko yako kupitia mfumo wetu huru na wa siri na wa kuaminika wa kutoa taarifa za manung’uniko wa, Your Voice.

Ukitoa taarifa ya manung’uniko, tunatarajia kwamba utakuwa umefanya hivyo kwa nia njema. Hii inamaanisha kwamba inabidi uwe na sababu nzuri za kufanya iaminike kwamba taarifa unayotoa ni ya kweli, hata kama baadae itakuja kua tofauti. Ukitoa kwa makusudi, taarifa ya manung’uniko ambayo ni ya uongo inayopotosha, inaweza kupelekea hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi yako.

Ni wakati gani napaswa kutoa taarifa nikiwa na manung'uniko?

Njia yoyote utakayoamua kutumia kutoa taarifa, unapaswa kuzungumza mapema badala ya baadaye. Ukisubiri au kuchelewa, kuna hatari ya hali kuwa mbaya zaidi, kwako na kwa JTI. Hii inaweza kusababisha ugumu kwenye kutatua.

Kitendo chochote cha kulipiza kisasi dhidi ya yeyote aliyetoa taarifa ya manung’uniko au aliyesaidia mchakato wa uchunguzi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Your Voice inafanyaje kazi?

Zungumza

Kuna njia mbalimbali za kutoa taarifa ukiwa na manung'uniko au za ukiukwaji wa maadili kupitia Your Voice.
  • Wasiliana na mtu wa kuwasiliana wa Your Voice
  • Tuma kwenye jukwaa la Your Voice mtandaoni
  • Au tuma barua pepe kwa Kitengo cha Maadili kupitia onebehavior@jti.com

Tathmini

Mtu wako wa kuwasiliana atawasilisha taarifa yako kwa Mwezeshaji katika timu ya kitengo cha Maadili, ambaye ataiangalia na kuamua juu ya hatua muafaka za kuchukua. Ikibidi, Kamati ya Maadili ya Biashara itaamua hatua sahihi za kufanya. Kama taarifa yako haipaswi kufanyiwa kazi kupitia Your Voice, Mtu wako wa kuwasiliana atakujulisha na kukushauri upeleke wapi taarifa yako ili ishughulikiwe.

Uchunguzi

Ikiwa uchunguzi zaidi utahitajika, utafanyika bila ya upendeleo na kwa haki na Kiongozi wa Upelelezi. Atawasilisha matokeo yao kwa mwezeshaji au Kamati ya Maadili ya Biashara. Ikibidi, Uongozi utashauriwa kuchukua hatua za kurekebisha hali iliyoripotiwa.

Hitimisho

Mtu wako wa kuwawasiliana atawajulisha matokeo ya uchunguzi. Kabla ya kesi yoyote kufungwa, Afisa Mkuu wa Utekelezaji Maadili anaitathmini.

Fahamu zaidi

Kilichopita Your guide