Wajibu wetu kwa jamii

Kutofungamana na upande wowote kisiasa

Kutofungamana na upande wowote kisiasa ni muhimu kwa maslahi yetu.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Hatutumii au kujaribu kutumia ushawishi usiofaa kwa mashirika ya kiserikali, wawakilishi au wabunge ili kuipa JTI upendeleo.

Tunaheshimu haki ya wafanyakazi ya kujihusisha na kushiriki kwenye michakato ya kisiasa endapo tu kujihusisha huko ni binafsi hakuhusishi JTI.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nafanya shughuli za kisiasa kwa wakati wangu na bila kutumia rasilimali za JTI, barua pepe au kuihusisha Kampuni kwa namna yeyote.

Situmii mahali pa kazi kufanya kampeni za kisiasa, kuomba usaidizi kutoka kwa wafanyakazi wengine au kutafuta michango ya fedha kwa shughuli zangu za kisiasa.

Nikidhamiria kushika nafasi kwenye ofisi ya umma, namwambia meneja wangu pamoja na Mshauri wa Kisheria wa eneo langu au wa kikanda.

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Hii ni baadhi ya mifano ya masuala yanayohusiana na shughuli za kisiasa:

  • Nataka kuhudhuria mkutano unaongozwa na mgombea wa bunge kwenye majengo ya JTI.
  • Nashiriki kikamilifu katika masuala ya siasa ya nchini kwangu nje ya kazi na ningependa kugombea uwenyekiti wa Serikai za mitaa.
  • Mfanyakazi mwenzangu anatumia gari lenye nembo ya kampuni kufanya shughuli za kisiasa.

Fahamu zaidi