Wajibu wetu kwa jamii

Kuheshimu Haki za Binadamu

Katika shughuli zetu zote za biashara, tunaheshimu haki za binadamu za wafanyakazi wetu, washirika wa biashara na wafanyakazi wao, na jamii tunazofanyia shughuli zetu.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Haki za kibinadamu ni kanuni za ulimwengu wote ambazo hutumika vilevile na kwa usawa kwa kila mtu, bila kujali wako wapi ulimwenguni, zikijumuisha mada kama fursa sawa, viwango vya kazi, uhuru wa kuzungumza na faragha.

Tunawapa watumishi wote taarifa za haki za binadamu kwa uwazi na tunafanya tathmini ya kutambua na kupunguza athari zinazoweza kutokea za masuala ya haki za binadamu.

Tunashirikiana na mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na makampuni binafsi ili kuboresha hali pale ambapo haki za binadamu zinaweza kuwa hatarini. Tunachukua tahadhari maalumu ili kupunguza hatari ya ajira ya watoto katika shughuli zetu na tunafanyia kazi ili kuondokana na ajira ya watoto katika jamii ambako ajira ya watoto inachukuliwa kama sehemu ya utamaduni.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nategemea JTI itaheshimu haki zangu za kibinadamu. Nikiwa na shaka juu ya ukiukwaji wa haki zangu za kibinadamu au wa wafanyakazi wenzangu, nasema.

Kama meneja, nina wajibu wa kuhakikisha kuwa haki za kibinadamu za wafanyakazi katika timu yangu zinaheshimiwa. Nashughulikia shaka yoyote inayoletwa kwangu na mfanyakazi kulingana na Mwongozo wa Mameneja.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Washirika wote wa biashara wanatarajiwa kufuata na kudumisha viwango vya kazi na mazingira ya kufanyia kazi vinayozingatia sheria zote za nchi na na mikataba ya kimataifa

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Hii ni baadhi ya mifano ya hali ambazo zinaweza kusababisha wasiwasi:

  • Nilipokuwa kwenye shamba la tumbaku, niliona mtoto amebeba mzigo mkubwa wa tumbaku.
  • Shirika lisilo la kiserikali linalojitegema linasema kwamba wafanyakazi wa shamba la tumbaku walikuwa wakifanya kazi bila vifaa vya kulinda usalama binafsi.
  • Nilisikia kwamba mfanyakazi mwenzangu aliombwa kufanya kazi siku za mwisho wa wiki bila HR kutaarifiwa.
  • Mfanyakazi mwenzangu amenyimwa haki ya kujiunga na umoja wa wafanyakazi na meneja wao.

Fahamu zaidi