Yaishi Maadii yetu

Mpendwa mfanyakazi,

Karibu kwenye toleo jipya la Mwongozo wa Maadili wa Kazi wa JTI. Limebadilishwa na sasa linapatikana kwa urahisi kwenye mtandao na kwa kupitia simu za mkononi.

Mwongozo huu wa Maadili una maana kwa kila mmoja wetu. Kwa baadhi yenu, mwongozo huu ni maelezo ya sisi ni nani kama Kampuni na viwango vya maadili tulivyoahidi kuvifuata. Kwa wengine, ni mwongozo wa kutusaidia kuamua nini cha kufanya kwenye kila hali. Kwangu, ni hivyo na pia ni ukumbusho wa kinachonifanya nijivunie kufanya kazi kwenye Kampuni hii kwa zaidi ya miaka 35.

Kiini cha Mwongozo wa Maadili ya Kazi kinatoa muhtasari wa ahadi zetu katika maeneo manne muhimu: watu wetu, bidhaa zetu, uadilifu wetu wa kibiashara na wajibu wetu katika jamii. Inaelezea kile kinachotarajiwa kwa kila mmoja wetu, bila kujali nafasi zetu za kazi kwenye Kampuni, idara au sokoni. Kwa hali ambazo haziko dhahiri Your Guide inaweza kukusaidia kufanya maamuzi na kujiamini kwamba umefanya uchaguzi sahihi.

Nawahimiza Mameneja wote, kuongoza kwa mfano na kuendeleza tabia ya uadilifu kwenye timu zao. Natarajia watatengeneza mazingira ambayo yanaendeleza uelewa na majadiliano ya uwazi, na yenye kuwapa wafanyakazi uhuru wa kuzungumza. Kwa kupitia ahadi yetu ya 'kufanya jambo sahihi' tu ndio tunaweza kutimiza malengo yetu ya biashara na kuhakikisha kuwa nia ya kweli ya JTI inatiliwa maanani na kutekelezwa.

Tumia Mwongozo huu wa Maadili katika kazi zako na wafanyakazi wenzako, washirika wetu wa biashara na wanaotupa huduma wakiwemo wasambazaji wetu, yajadiili, yaelewe na muhimu zaidi, yaishi. Kila siku.

Timu moja. Mwenendo Mmoja. Mafanikio Yetu.


Howard Parks
Makamu wa Rais Mwandamizi, Rasilimali Watu na Afisa Maadili Mkuu

“Tumia Maadili haya katika kazi zako na wafanyakazi wenzako, washirika wetu wa biashara au wanaotupatia huduma wakiwemo wasambazaji wetu, yajadiili, yaelewe na muhimu zaidi, yaishi.”

Kilichopita Karibu kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu
Kinachofuata Kuhusu Mwongozo huu