Vigezo na Masharti

Tovuti hii inaendeshwa na JT International SA. Kwa kutumia tovuti hii unakubali Vigezo& Masharti na Tamko la kuzingatia Faragha vilivyowekwa hapa chini. Ikiwa hukubaliani na vigezo hivi, acha kutumia tovuti hii mara moja.

Vigezo na masharti haya yanatumika kwa ya tovuti ya WWW.CODEOFCONDUCT.JTI.COM.

1.1 Kukubali Masharti haya

Tovuti yetu inapatikana duniani kote kwa mtu yeyote anayepata Intaneti. Upatikanaji na matumizi ya tovuti yetu yanazingatia vigezo na masharti haya. KUTUMIA NA KUPATA TOVUTI YETU, UNAKUBALI, BILA MIPAKA, VIGEZO NA MASHARTI HAYA YOTE. Tuna haki ya kubadili vigezo na masharti haya wakati wowote. Mabadiliko ya vigezo na masharti haya yatatokea kwa kufungua tu toleo jipya na lililobadilishwa la vigezo na masharti kwenye tovuti yetu. Kwa kutumia mtandao wetu, unakubali tangu mwanzo kabisa kwamba matumizi yote yatatii vigezo na masharti.

1.2 Dhumuni la Tovuti hii

Tovuti hii inaendeshwa kwa madhumuni ya kutoa habari kuhusu Maadili ya Kazi ya JT International.

1.3 Umiliki wa Nyenzo, Hakimiliki na Notisi ya Alama za Biashara

Nyenzo zote zilizotumika na kuonyeshwa kwenye tovuti yetu, ikiwa ni pamoja na maandishi, programu, picha, vielelezo na michoro, video, muziki na sauti, majina, nembo na alama za biashara ni mali ya JT International S.A. (JTI) na ndio pekee mwenye kibali cha umiliki na vinalindwa na hakimiliki, nembo za biashara na sheria nyingine. Tovuti inaweza kujumuisha alama za biashara za wadau wetu. Alama hizi za biashara ni mali ya wamiliki husika, na unakubaliana kutozitumia au kuzionyesha kwa namna yoyote bila idhini ya maandishi ya wamiliki wa alama husika. Unaruhusiwa kupakua nyenzo kutoka tovuti yetu tu kwa ajili ya matumizi yako binafsi, yasiyo ya kibiashara, lakini katika kufanya hivyo usiondoe au kurekebisha alama yoyote ya biashara, hakimiliki au taarifa nyingine ya wamiliki. Unakubaliana kutotengeneza, kutumia tena, kupeleka kwa wengine, kusambaza kwa njia ya kieletroni, kusambaza kwa njia isiyo ya kielektroni, kuuza, kuchapisha, kutangaza au kueneza nyenzo hizi bila ruhusa ya maandishi kutoka JTI. Hauruhusiwi kutumia makabrasha haya kwenye tovuti yetu inayopatikana kama sehemu ya tovuti nyingine kwa kuunganisha, kuandaa au njia nyingine yoyote. Haki zozote zisizopewa kwa uwazi hapa zimehifadhiwa.

1.4 Viunganishi

JTI haipitii au kufuatilia nyenzo zilizomo kwenye tovuti zilizounganishwa kwenye tovuti yetu na hatuwajibiki na maudhui ya tovuti hizi zilizounganishwa na yetu. Kujiunganisha na tovuti hizo na hatari yoyote inayoweza kutokea kwa kufanya hivyo ni ya kwako binafsi.

1.5 Tamko la kuzingatia Faragha

Tafadhali bofya hapa kuona na kupitia tamko la kuzingatia Faragha ya tovuti ya WWW.CODEOFCONDUCT.JTI.COM iliyoingizwa kwa kumbukumbu katika Vigezo na Masharti haya. Kwa kukubali Vigezo na Masharti haya, unakubali kuwa unafungwa na matamko ya faragha na kwamba umepata maelezo ya kina na ya kutosha kuhusu kushughulikia data zako binafsi. Ukitaka kupata maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana nasi.

1.6 KANUSHO LA DHAMANA

TOVUTI YETU IMETOLEWA ‘KAMA ILIVYO’ BILA DHAMANA YA AINA YOYOTE ILE, KWA KUJIELEZA AU KWA KUASHIRIA, IKIJUMUISHA KUTOKUWA NA DHAMANA YA JINA, DHAMANA ZA KUUZA AU DHAMANA YA TOVUTI KUFAA KWA MATUMIZI MENGINE. JTI HAIWAJIBIKI KWA USAHIHI AU UTHABITI WA KUAMINIKA KWA TAARIFA ZA UKWELI, MAONI, USHAURI AU MATAMKO KWENYE TOVUTI. MAKALA ZOTE NA NYENZO ZINAZOONEKANA KWENYE TOVUTI NI YA TAARIFA TU NA HAZICHUKUI NAFASI YA USHAURI MAALUM.

1.7 UKOMO WA UWAJIBIKAJI

HATARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA KWA MATUMIZI YA TOVUTI YETU NI YAKO BINAFSI. SI JTI WALA, KAMPUNI MAMA, JAPAN TOBACCO INC. AU KAMPUNI ZAKE TANZU ZOZOTE, WASHIRIKA, MAWAKALA, WAWAKILISHI, AU WATOA LESENI HAWANA WAJIBU KWAKO AU KWA MWINGINE YEYOTE KWA UPOTEVU AU MADHARA/MAJERAHA AU HASARA ZA MOJA KWA MOJA/ ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA, ZINAZOTOKANA NA, ZA KIPEKEE, ZA KUADHIBU AU ZINAZOFANANA NA HIZO ZITAKAZOJITOKEZA KUTOKANA NA WEWE KUWEZA AU KUTOWEZA KUINGIA KWENYE TOVUTI YETU AU KUITUMIA, TOVUTI YETU AU TAARIFA ZILIZOPO KWENYE TOVUTI YETU AU MATENDO AU HALI ZITAKAZOTOKANA AU KUFUATIA TAARIFA ZA KWENYE TOVUTI. HIVYO BASI UNAONDOA AINA YOYOTE YA MASHTAKA DHIDI YA JTI, JT NA KAMPUNI TANZU ZAKE, VITENGO, WASHIRIKA, WAWAKILISHI NA WATOA LESENI YATAKAYOTOKANA NA MATUMIZI YA TOVUTI YETU NA TAARIFA ZILIZOPO.

1.8 Ukomo

Sehemu yoyote ya vigezo na masharti ikitangazwa na mahakama au mamlaka ya sheria kwamba hayafai au hayawezi kutumika, haitaathiri uhalali wa matumizi wa sehemu yoyote iliyobaki ya vigezo na masharti haya na sehemu hiyo iliyobaki itabaki na uwezo na athari kamili.

1.9 Utatuzi wa migogoro

Vigezo na masharti haya na migogoro yoyote inayotokana na au kuhusiana na tovuti yetu inasimamiwa, na kutajwa na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria za Uswisi. Mahakama na mabaraza ya mahakama ya jimbo la Geneva, Uswisi, wana mamlaka ya kipekee ya kisheria.

2. Faragha na Sheria

Tovuti hii inaendeshwa na JT International SA. Kwa kutumia tovuti hii unakubali Tamko la Faragha na Vigezo na Masharti yaliyo hapa chini. Kama hukubaliani na sera hizi, acha kutumia tovuti hii mara moja.

2.1 Tamko letu kuhusu Faragha

Tamko hii la faragha (“Tamko”) linatumika kwa taarifa iliyotolewa na Mtumiaji kwa WWW.CODEOFCONDUCT.JTI.COM.

Kwa sababu faragha yako ni muhimu kwetu, tunataka kuonyesha dhamira yetu kwa faragha yako na kwa hiyo, tumekubaliana kutoa taarifa za sharia zetu na utendaji. Taarifa zote utakazotoa kwetu zitakuwa chini ya kanuni na misingi iliyoainishwa kwenye Tamko.

Maswali na maoni yote yanayohusiana na sera yetu ya faragha yaelekezwe kwenye ukurasa wa Mawasiliano wa www.jti.com.

Kwenye tovuti yetu tunakusanya taarifa kwa njia tofauti:

2.2 Mafaili ya taarifa ukiingia kwenye tovuti

Kila unapojiunga kwenye tovuti yetu, tunakusanya taarifa fulani kuhusu uhusiano wako na kompyuta yako. Hii ni pamoja na anwani yako ya IP, aina ya kivinjari chako na mipangilio, aina ya kompyuta yako na mifumo ya uendeshaji unayotumia. Tunatumia anwani za IP ili kuchambua mwenendo, kusimamia tovuti, kufuatilia harakati za mtumiaji, na kukusanya taarifa za watu wa jumla kwa matumizi ya jumla. Habari zilizokusanywa katika faili wakati unaingia kwenye tovuti hazihusishwi na taarifa za kibinafsi

2.3 Vibwedo

Vibwedo ni sehemu ya data iliyohifadhiwa kwenye kompyuta yako, yenye habari inayoongeza na kuwezesha kuperuzi kwenye tovuti yetu. Matumizi ya vibwedo hayataunganishwa na taarifa yoyote ya kibinafsi wakati ukiwa kwenye tovuti yetu.

Umiliki wa Taarifa

JTI hukusanya taarifa zote unazozitoa kupitia tovuti  yetu, na ndiye mmiliki pekee wa habari zilizokusanywa kwenye tovuti hii.

KWA KUTUPA TAARIFA ZAKO ZA KIPEKEE ZA KUKUTAMBUA, UNATURUHUSU KUTUMIA TAARIFA HIZO KWA MUJIBU WA SHERIA NA KANUNI ZA TAMKO.

Ukitupa habari nyingine kama vile mapendekezo kuhusu tovuti au bidhaa zetu, au mapendekezo mengine yoyote, mawazo au habari, taarifa hiyo itakuwa yetu na tunaweza kuitumika na kuifichua kwa namna yoyote tunayochagua, bila kukulipa fidia yoyote.

2.5 Viunganishi

Tovuti hii inaweza kuwa na viunganishi kwenye tovuti nyingine. Tafadhali unatahadharishwa kwamba hatuwezi kuwajibika kwa utendaji wa faragha wa mitandao mingine. Tunakuhimiza kuwa makini pindi utokapo kwenye tovuti yetu na soma matamko ya faragha ya kila tovuti ambayo inakusanya taarifa za kibinafsi za kukutambua. Tamko hili linatumika kwa habari iliyokusanywa na sisi tu kupitia tovuti hii.

2.6 Mabadiliko katika Tamko letu kuhusu Faragha

Tuna haki ya kubadilisha sera yetu ya faragha wakati wowote kwa kutuma sera iliyorekebishwa kwenye tovuti. Ni wajibu wako kuangalia mara kwa mara mabadiliko yoyote tunaweza kufanya kwa sera hii. Ikiwa hukubaliana na mabadiliko katika sera yetu, tutumie barua pepe inayoomba kufuta habari yoyote uliyokwishaitoa na tutaheshimu matakwa yako. Kuendelea kutumia tovuti hii baada ya kuweka mabadiliko inamaanisha unakubaliana na mabadiliko hayo.

 

Kinachofuata Karibu kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu