Wajibu wako kama meneja

Wakati Maadili yetu, sera na kanuni zinatumika kwa wafanyakazi wote, kama meneja, tunatarajia utaweka mfano mzuri kwa kuyaishi maadili ya JTI na kuhamasisha wengine kuwa na tabia zenye maadili mema na zenye uwajibikaji wakati wote.

Kama meneja, una jukumu muhimu katika kukuza ufahamu wa Maadili yetu ndani ya timu yako. Ni muhimu kwa kila mtu kuelewa kinachotarajiwa kutoka kwake na kupata mafunzo na mwongozo sahihi ili kufanya maamuzi ya kimaadili yaliyo sahihi.

Tunakutegemea kwenye kujenga mazingira ya kazi ambapo watu wote kwenye timu watahisi wepesi kuelezea wasiwasi au mashaka waliyonayo na kujua wazungumze na nani kuhusiana na mashaka yao. Mfanyakazi akija kwako akiwa na wasiwasi au mashaka ya aina yoyote, tunatarajia utampa uzito na umakini unaostahili na kumsaidia kutatua suala hilo kwa kujiamini na bila hofu ya kulipiziwa kisasi. ‘Mwongozo wa mameneja wa kushughulikia taarifa za utovu wa nidhamu zinazotolewa pale ambapo mfanyakazi ana mashaka au wasiwasi’ unapatikana ili kukusaidia, endapo hali hiyo itatokea.

Kwenye kipengele kinachofuata, utapata zana za kukusaidia kuboresha tabia ya uadilifu ndani ya timu yako. Zana hizi zinajumuisha mwongozo mfupi, hali za kimaadili zenye utata na zaidi, ambazo tutaziboresha kila baada ya muda.

Kama unasoma nakala iliyochapishwa ya Maadili haya na huwezi kupata zana hizi, tafadhali wasiliana na HR Business Partner nchini kwako au mjumbe wa timu ya kitengo cha Maadili.

Kilichopita Kuhusu Mwongozo huu
Kinachofuata Your guide