Karibu kwenye Mwongozo wa Maadili yetu ya Kazi

Mpendwa mfanyakazi,

Kutimiza lengo letu la kuwa #1 haliwezi kutekelezwa kwa gharama yoyote. Tutafanikiwa tu kwa kufanya kazi ndani ya mfumo wa Maadili yetu ya Kazi na kwa kufanya mambo sahihi siku zote.

Mara nyingi nayachukulia Maadili ya Kazi kama dira, inayoniongoza mwelekeo sahihi pale ninapokuwa na shaka. Nakushawishi kuutumia kama mwongozo, na ikiwa hutopata majibu unayotafuta, tafuta ushauri. Sifa na mafanikio ya msingi ya kampuni yetu yanategemea kwa kila mmoja wetu kufanya kazi kwa ubora wa juu zaidi, na kwa lengo moja.

Wakati tunafanya kazi kwenye kampuni yenye uanuwai wa kweli, tunapaswa kuzingatia viwango vya kimaadili vinavyofanana na maadili ya Kampuni yetu. Mwongozo huu unaunga mkono matarajio haya kwa kutuongoza namna tunavyofanya kazi na kuthibitisha kile kinachotutofautisha na wengine.

Kwa namna fulani, ingawa Mwongozo huu unamlenga mtu mmoja mmoja, pia unaimarisha ari ya 'Timu moja'. Uamuzi wowote unaweza kuwa na athari kubwa kwa yale yaliyojengwa na wengine - kila mmoja wetu ana jukumu binafsi kuchangia katika mafanikio yetu ya pamoja.

Kwahiyo nakuomba uwe kinara wa kuzingatia Mwongozo huu wa Maadili ya Kazi ya JTI. Sio ngumu, ujumbe uliomo unahitaji busara ya kawaida tu. Utumie, kama mimi, ili kuelewa vizuri Kampuni yetu inahusu nini na mwisho wa siku ya kazi jikumbushe kwamba ulifanya jambo sahihi.


Eddy Pirard
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu

“Kutimiza lengo letu la kuwa #1 haliwezi kutekelezwa kwa gharama yoyote.”

Kinachofuata Kuhusu Mwongozo huu