Uadilifu wetu wa biashara

Kuepuka migongano ya maslahi

Tunategemea wafanyakazi wataepuka hali yoyote ambapo maslahi yao binafsi yanaweza kupingana na yale ya JTI.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Migongano ya maslahi inaweza kuwashawishi wafanyakazi kufanya maamuzi ambayo hayana maslahi kwa JTI na inaweza kuathiri vibaya sifa ya Kampuni pamoja na yao wenyewe.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Naepuka hali ambapo migongano ya maslahi inaweza kutokea.

Siziruhusu maslahi yangu binafsi kuathiri maamuzi yoyote ninayofanya kwa niaba ya JTI. Natoa taarifa ya uhusiano wowote wa familia au wa kibinafsi ambao unaweza kuathiri maamuzi yangu kwenye kazi.

Nje ya kazi, sijihusishi na shughuli yoyote ambayo inaweza kudhoofisha au kushindana na maslahi ya biashara ya JTI.

Pia nakumbuka migongano ya maslahi inayoweza kutokea wakati wa kubadilishana zawadi, ukarimu au burudani.

Pale ambapo mgongano wa maslahi hauwezi kuepukika, natoa taarifa mara moja kujilinda mwenyewe na kuilinda JTI.

Kama meneja, nina wajibu wa kushughulikia mgongano wowote wa maslahi nilitaarifiwa na mtu yeyote kwenye timu yangu, kwa msaada wa timu za HR na kitengo cha Maadili.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Washirika wa biashara wanapaswa kuepuka hali yoyote ambayo inaweza kusababisha mgongano wa maslahi. Migongano yoyote ya maslahi inayoweza kutokea na JTI ni lazima kutoa taarifa kupitia onebehavior@jti.com.

Haya yanaweza kutumika kwenye mazingira gani?

Hii ni baadhi ya mifano ya migongano ya maslahi inayoweza kutokea:

  • Kaka yangu anaomba nafasi ndani ya JTI, na mimi nitakuwa sehemu ya mchakato wa kufanya maamuzi ya kumchagua.
  • Mtoa huduma anayegombea zabuni ya JTI, ambayo nitakuwa sehemu ya mchakato wa kuchagua mshindi amelipia hoteli ya kifahari nikajivinjari mwisho wa wiki.
  • Ili kupata kipato cha ziada, nilijiandikisha kufanya utafiti nje ya saa zangu za kazi, kazi ya kwanza ikawa juu ya maendeleo ya teknolojia kwa ajili ya kutumia kwenye sekta ya tumbaku.

Fahamu zaidi