Uadilifu wetu wa biashara

Kuheshimu faragha na usiri

Tunahakikisha tunakusanya, kutumia na kuhifadhi taarifa zetu binafsi kihalali na kiusalama. Tunafanya hivyo hivyo kwenye taarifa zetu za siri.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Katika shughuli zetu zote, tunakusanya na kushughulikia taarifa binafsi zinazohusiana na wafanyakazi wetu, washirika wa biashara na wadau wengine. Tuna wajibu wa kuchunguza habari hizo kwa makini na kwa siri na kufanyia kazi taarifa ambazo ni muhimu kwa ufanisi wa utendaji wa JTI tu.

Pia tunatengeneza taarifa za biashara kuhusu Kampuni yetu, zinazohitaji usiri wa kiwango hicho.

Utoaji wa taarifa binafsi za siri kunaweza kuharibu sifa yetu na kutuathiri vibaya kibiashara.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nakuwa makini na taarifa binafsi. Siku zote naheshimu faragha za wahusika na kutumia habari kihalali.

Nakuwa makini sana kwenye kutoa taarifa binafsi. Na nazitoa tu kukiwa na sababu halali inayohusiana na biashara. Nikiwa na shaka, naomba mwongozo kutoka kwa Mshauri wa Sheria wa kanda au nchini.

Natumia vifaa na mifumo salama iliyoruhusiwa na IT ya JTI kuhifadhi na kutoa taarifa za siri na binafsi. Naweka vifaa na nyaraka zangu salama, pia naweka nywila ngumu na salama za kufikia mifumo ya JTI IT, tovuti na mali nyingine za kampuni.

Nakuwa makini zaidi nikifanya kazi nje ya majengo ya JTI ili kuhakikisha watu wasioidhinishwa hawasikii, kuona au kupata taarifa za siri au nywila.

Nikipokea taarifa za siri na sijui zilikotokea au lengo la taarifa hizo, nazungumza na meneja wangu. Huwa sijibu ujumbe wa kuomba taarifa za siri na sifungui kiunganisho au viambatanisho kwenye ujumbe huo.

Natoa taarifa mara moja juu ya uvunjaji wowote wa usiri unaohisiwa au matumizi mabaya ya taarifa kwa Mshauri wa Sheria wa kanda yako au wa nchini, au mjumbe wa timu ya kitengo cha Maadili au timu za Usalama wa taarifa.

Ni taarifa gani zinazungumziwa hapa?

Taarifa binafsi ni taarifa zozote zinazohusiana na mtu binafsi, kwa mfano jina, anwani, maelezo ya mawasiliano, nambari za kitambulisho, na maelezo kuhusu afya, familia, fedha au kazi zao.

Taarifa za siri ni pamoja na habari zinazohusiana na shughuli zetu, bidhaa, mipango ya biashara, washirika wa biashara, ambazo zikitolewa zinaweza kuharibu biashara ya JTI au sifa yake.

Fahamu zaidi