Bidhaa zetu

Kushirikiana na washirika wa biashara

Washirika wetu wa biashara ni muhimu sana kwa mafanikio yetu. Wanachaguliwa kwa umakini kulingana na vigezo maalumu ikiwa ni pamoja na kufuata kwao sheria na kanuni, uadilifu wa biashara, ubora, afya na usalama, haki za binadamu, viwango vya kazi na usimamizi wa mazingira.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Washirika wetu wa biashara ni pamoja na wateja wetu, wasambazaji, wakulima, wafanyabiashara wa tumbaku, wasambazaji na wadau wengine tunaohusiana kibiashara.

Mwenendo usiofaa wa washirika wetu wa biashara unaweza kuathiri sifa yetu. Tunahakikisha kwamba tunafanya kazi na washirika wanaozingatia viwango vya juu vya maadili.

Wadau wote wanaotupatia huduma wanatakiwa kutoa huduma hizo kulingana na Viwango vya JTI, na viwango hivi ndivyo hutumika kuwachagua na kushirikiana nao.

Sheria za Kilimo za JTI (ALP) zinalenga kuboresha namna shughuli za wakulima na wafanyabishara wa tumbaku zinavyofanyika, zinaongelea pia mada kama haki za wafanyakazi, afya na usalama na ajira za watoto.

Tunafanya bidii kuhakikisha kwamba washirika wetu wote wa biashara wanaonunua au kushughulikia bidhaa zetu za tumbaku wanadumisha sifa yetu ya uaminifu na uadilifu.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nasaidia jitihada za JTI kudumisha viwango vya juu katika ugavi wetu, kwa kudumisha mahusiano mazuri na washirika wa biashara, kujenga matarajio yanayojulikana na pande husika na kuheshimiana.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Tunategemea washirika wetu wa biashara wataheshimu sheria, kuzingatia maadili ya kufanya biashara na kuzingatia viwango vyetu vya juu.

Wakulima wote na wafanyabiashara wa tumbaku wanahimizwa kuzingatia utekelezaji wa Sheria za Kilimo za JTI (ALP), na JTI inaweza kutoa msaada katika uzingatiaji wa programu za ALP.

Kutekeleza Sheria za Kilimo

Wakati wa kulima tumbaku, moja ya wataalamu wetu wa kilimo alikuwa anamtembelea mkulima kama kawaida. Akiwa kwenye moja ya ziara hizo alikuta mkulima ananyunyizia dawa za kulinda mazao dhidi ya wadudu waharibifu bila kuvaa vifaa alivyopewa na JTI vya kujikinga na madhara ya dawa hizo. Mtaalamu alimwelezea hatari za afya na usalama anazoweza kupata kwa kutotumia vifaa hivyo na jinsi gani vifaa hivyo vinavyoweza kumsaidia kumlinda. Akamwalika mkulima huyo kwenye mafunzo ya matumizi ya vifaa vya kujikinga yaliyokua yanatolewa kwenye eneo lake kwa kushirikiana na JTI. Muda mwingine wa kunyunyizia dawa za kulinda mazao dhidi ya wadudu waharibifu ulipofika, mtaalamu wetu alifurahia kuona mkulima huyu akifanya hivyo akiwa amevaa vifaa vyake vya kujiinga.

Fahamu zaidi