Wajibu wetu kwa jamii

Kuhakikisha ushindani wa haki

Tunahakikisha kwamba tunashindana kwa haki kwenye masoko yote na kwa kufuata kiadilifu sheria zote za ushindani.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Tabia yoyote ambayo ina madhumuni au athari ya kupotosha ushindani wa haki, ni ushindani kinzani.

Kutozingatia sheria za ushindani wa haki, hata bila kukusudia, inaweza kusababisha adhabu kali kwa JTI na wafanyakazi wake.

Tunafanya shughuli zote na maamuzi ya kimkakati bila kutegemea washindani wetu. Tunaheshimu kwamba wateja wetu wanapaswa kuwa huru kufanya maamuzi yao ya biashara kuhusu wateja wao na jinsi wanavyoshindana katika soko.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nina wajibu wa kujua sheria za ushindani wa haki na kuwa na ufahamu wa mipaka waliyoweka.

Katika shughuli zote, naamua mkakati wa kibiashara wa JTI na vitendo kwa kujitegemea bila kuhusisha washindani. Nafanya maamuzi kwa maslahi ya JTI tu, na bila ya kushauriana, ushirikiano au makubaliano na washindani, wala kubadilishana taarifa za siri.

Nahakikisha kwamba wateja wanabakia na uhuru wa kufanya maamuzi ya biashara yao, kuhusiana na wateja wao na tabia za kushindana katika soko.

Nashughulika na kuwasiliana taarifa nyeti za ushindani kwa umakini wa hali ya juu na kuhakikisha usalama wake unalindwa na kutunzwa.

Nashauriana na mshauri wa timu ya Sheria mara moja ikiwa naona tukio lolote la shughuli za kukinzana na ushindani wa haki katika eneo la biashara yangu, au nikiwa na maswali yoyote kuhusu sheria za ushindani na jinsi yanavyohusiana na kazi yangu.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Washirika wa biashara, ikiwa ni pamoja na washauri na wauzaji wa data, wanawajibika kwa kuzifahamu sharia husika za ushindani na kutunza siri na taarifa nyeti za ushindani.

Kumbuka:

  • Kua makini kwenye kushughulikia barua pepe na ujumbe wa maandishi kama barua au mkataba kama unavyokua makini kwenye mazungumzo ya ana kwa ana.
  • Fanya mikutano ya vyama vya biashara kwa njia ile ile kama mikutano ya washindani.
  • Weka kumbukumbu sahihi ya kile kilichojadiliwa wakati wa mikutano na washindani, vyama vya biashara au vikundi vya sekta.

Fahamu zaidi