Wajibu wetu kwa jamii

Kulinda mazingira

Biashara yetu inategemea ugavi endelevu ikiwa ni pamoja na sehemu kubwa inayohusiana na kilimo. Tunahakikisha kwamba tunapunguza madhara kwa mazingira ya shughuli zetu, kutunza rasilimali kwa vizazi vijavyo.

Hii ina maana gani kwa JTI?

Tunasimamia majukumu yetu ya kulinda mazingira na tumejizatiti kwenye maboresho endelevu na uwazi wa ufanisi wetu.

Biashara yetu na ugavi wetu unaweza kupata tishio la mabadiliko ya hali ya hewa, kuisha kwa rasilimali za asili, uhaba wa maji na kuharibika kwa mazingira.

Tunahakikisha kwamba tunapunguza matumizi yetu ya nishati na uzalishaji wa kaboni dioksidi kupitia mipango ya kupunguza na kuwekeza katika nishati mbadala. Pia tunazingatia kupunguza matumizi yetu ya maji na kupunguza taka katika shughuli zetu. Hii ni pamoja na kuwekeza katika mafunzo, ujuzi na mipango ya kupunguza matumizi makubwa ya nishati.

Tunaangalia hatari kwa mazingira katika ugavi wetu, na kuchukua hatua za pamoja kupunguza hatari hizi kupitia utaratibu wetu wa manunuzi na kwa kushirikiana na wauzaji wetu, wakulima wa tambaku na wadau wengine.

Hii ina maana gani kwangu kama mfanyakazi?

Nikifanya kazi zangu za kila siku nadhamiria kupunguza athari inayoweza kutokea kutokana na nishati, maji na vifaa navyotumia. Nazingatia athari kwa mazingira nikiwa nafanya maamuzi ya biashara. Nikiwa sina uhakika uamuzi wangu unaweza kuathiri mazingira kwa kiasi gani, nazungumza na mwakilishi wa EHS nchini.

Kama meneja, nina wajibu wa kuboresha tabia za kulinda mazingira ndani ya timu yetu na kuhakikisha taratibu husika za kulinda mazingira zinafuatwa. Nashiriki kwenye programu zenye lengo la kuboresha utendaji wetu unaoathiri mazingira kwa namna chanya.

Hii ina maana gani kwa washirika wetu wa biashara?

Washirika wetu wa biashara wanatarajiwa kuwa na udhibiti wa usimamizi wa kupunguza hatari kwa mazingira na kupunguza vikwazo vya mazingira. Tunahamasisha washiriki wetu wa biashara kufanya kazi nasi kutambua na kushughulikia changamoto za mazingira katika mlolongo wetu wa uzalishaji.

Nawezaje kuongeza ushiriki wangu?

  • Kutambua na kupendekeza fursa za kupunguza matumizi ya nishati k.m. rasilimali, vifaa na taka
  • Tumia nishati na maji kwa uangalifu na uzime na kufunga wakati havitumiki
  • Sishiriki katika shughuli zaa mazingira nchini
  • Kuwasilisha miradi ya mazingira iliyotekelezwa kwenye tuzo za JTI za ‘annual Sustainability Awards’

Fahamu zaidi