Maamuzi unayofanya yanaweza kutuathiri sisi wote.

Your guide ni mwongozo wako wa kufanya maamuzi kiadilifu

Maamuzi unayofanya yanaweza kutuathiri sisi wote.

Kila mmoja wetu ana jukumu muhimu katika kuzingatia viwango na maadili ya JTI, kuhakikisha kuwa JTI ni sehemu nzuri ya kufanya kazi na kulinda sifa yetu.

Katika shughuli zako za kila siku, mara nyingi uamuzi sahihi utakua dhahiri kwako, kulingana na ufahamu wako wa maadili yetu, Mwongozo wa Maadili yetu ya Kazi na sera na kanuni nyingine za kampuni. Busara zako za kawaida zinaweza pia kukusaidia kuamua kipi ni sahihi.

Hata hivyo, wakati mwingine, unaweza kukabiliana na mazingira ambapo hujui nini ni sahihi kufanya. Katika hali kama hizi, ‘Your Guide’ inakuongoza kupitia mchakato wa uamuzi, kukuwezesha kuzingatia mambo yote muhimu na nini cha kutarajia kutokana na uamuzi wako.

‘Your Guide ’ni zana rahisi ya kutumia kukusaidia kufanya uamuzi sahihi kwako na kwa JTI.

Ukihisi kuna kitu au hali ambayo haiko sawa...

Mfano, hauna uhakika kuhusu kitu fulani:

 • Ulichopanga kufanya
 • Ulichoombwa kufanya
 • Ulichoona au kusikia

Jiulize: Kuna tatizo?

Utajisikiaje kuhusu kitu hiko, endapo:

 • Utakiona kwenye vyombo vya habari?
 • Watu wako wa karibu watakisikia?

Angalia:

 • Kinazingatia sheria?
 • Kinaendana na Maadili ya Kampuni na Mwongozo wetu wa Maadili?
 • Kinaendana na maadili yako binafsi?

Ukihisi una amani

Endelea

Bado una mashaka au hauna uhakika?

Omba ushauri kutoka kwa mmoja wa wafuatao:

 • Meneja wako
 • HR business partner wako
 • Mshauri wa Sheria nchini
 • Mjumbe wa kitengo cha Maadili
Kilichopita Wajibu wako kama meneja
Kinachofuata Kutoa taarifa ukiwa na manung’uniko